Niki Mbishi awavaa wasanii hawa
Rapa Nikki Mbishi amefunguka na kuwachana baadhi ya wasanii
wanaojifanya kuwa ni wasanii wakubwa ili hali hakuna uwekezaji wowote
ambao wameufanya na kusema wasanii wengi wa Bongo ni waganga njaa.
Niki
Mbishi amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kudai kuwa
hivi sasa wasanii wengi wa Bongo fleva wamekuwa wakilialia sana kwenye
Interview zao
"Siku hizi wasanii wa Bongo flavor kwenye Interviews
wanalia tu, sijui wameukosea nini mfumo wao au Miungu yao (Mameneja
Uchwara)? Kheri kufa macho kuliko kufa moyo, by the way sisi wengine
tunaambiwa hatupo kwenye A-LIST ya wasanii wa Hip Hop kama hao
wanaoonekana wana mafanikio. Nilifanya Interview na Duwe Sentana
akaniuliza kwanini sipo kwenye A-LIST nami nikamtaka anitajie wasanii
wawili tu wa Hip Hop walio kwenye huo udwanzi wanaodanganyana,
akanitajia jamaa kama wanne hivi, nikamuuliza hao jamaa ndo wenye
mafanikio? Akasema ndio wanapata endorsements za makampuni, wanafanya
shows nyingi yaani kifupi wanapiga hela, nikamuuliza wamefanya uwekezaji
gani (Investment)? Maana wanapaswa wawe ma-CEO wa kampuni zenye uwezo
mkubwa kihamasa na kifedha sio kuwa ass kissers na ubabaishaji mwingi"
Niki Mbishi aliendelea kusema kuwa
"By the way jikune mkono wako unapofika usilazimishe
usipofika utahadhirika, wasanii wengi ni waganga njaa tu maana hawana
cha kuonesha wala kujivunia tofauti ya views, comments na likes za
mitandao ya kijamii. Nani yupo kwenye A-LIST ya hip hop ajaze uwanja
peke yake tumuone ikiwa ukimuweka hata Maisha Basement hajazi. Acheni
kutaka u Jay Z na u Puff Daddy ikiwa hamna sauti ya mamlaka juu ya kazi
zenu" alisisitiza Niki Mbishi
Niki Mbishi wiki kadhaa alifanya Interview kwenye kipindi cha eNewz
na kutaja wasanii kama Joh Makini, Fid Q, AY kuwa ni mfano wa rappers
ambao wapo kwenye A list na kuwa na mafanikio kutokana na kazi yao ya
muziki hapa Bongo.
Post a Comment