Lema amuomba Rais Magufuli
Mbunge
wa Arusha Mjini, Gobless Lema amefunguka na kumuomba Rais Magufuli
kuwasaidia askari polisi wa Arusha na Tanzania kiujumla kuwaboreshea
makazi yao kwa kuwajengea nyumba bora kwani anadai polisi walio wengi
wanaishi nyumba za hali ya chini sana
Lema alisema hayo jana na kusema kuwa ni aibu kubwa kuonekana polisi
wanachangiwa pesa ili kuweza kufanya marekebisho katika nyumba ambazo
ziliteketea kwa moto juzi jijini Arusha.
"Mimi
ni wito wangu kwa askari polisi pamoja na mchango wake kwa polisi hao
lakini namwambia tu askari polisi nchi nzima wanaishi kwenye nyumba
zenye hadhi ya chini sana, serikali inaweza kufanya 'commitment'ikajenga
nyumba za maana maghorofa na askari wote wanaoishi mtaani wakarudi
kuishi hapo, ni aibu kwa jeshi la polisi kutembeza kibaba kwa ajili ya
kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga nyumba za askari polisi hao watu
wanakesha usiku na mchana kulinda usalama wa watu na mali zao hawa watu
hawatakiwa kufanyiwa 'donation'" alisema Godbless Lema
Aidha Mbunge huyo anasema yeye anaamini serikali inaweza kuchukua jukumu
la kujenga nyumba za polisi Arusha tena kwa haraka kama ambavyo Rais
Magufuli aliamua kujenga hostel za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) kwa kipindi kifupi sana.
Post a Comment