Ester Bulaya hatarini
Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini kupitia tiketi ya CHADEMA, Ester Amos
Bulaya, amesema yupo katika hatari kubwa kutokana na kufuatiliwa na watu
ambao anahisi sio wazuri huku wakiwa wamevalia mavazi ya ninja,
nyumbani kwake wilayani Bunda.
Bulaya
ameto taarifa hiyo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa
Television, na kusema kwamba watu hao walimfuata nyumbani kwake wakiwa
na gari ya Noah huku wamevalia kinija, bahati nzuri hakuwepo nyumbani
hivyo ndugu zake wakamwambia asirudi nyumbani siku hiyo.
Ester Bulaya ameendelea kuelezea kwamba watu hao walizunguka kwa
baadhi ya ndugu zake akiwemo bibi yake na kumkosa, lakini alienda kutoa
taarifa polisi na mkuu wa kituo kuanza kufuatilia suala hilo, lakini
haikuchukua muda akahamishwa kituo cha kazi.
Post a Comment