Header Ads

"Ndoa yangu haihusiani na siasa" - Kafulila

Daudi Kafulila ambaye hapo jana amekihama chama cha CHADEMA, amesema suala la mke wake kuridhia au kutoridhia kwa yeye kuhama chama wakati yeye ni Mbunge wa chama hiko, ni suala ambalo halihusiani na ndoa yao.
Kafulila ameyasema hayo leo na kueleza kwamba linapokuja suala la ndoa hapo ndio huwa lazima wafikie makubaliano, lakini ikija suala la kisiasa kila mtu ana uamuzi wake ambao hawaingiliani kwani ndoa yao ilifngwa kanisani na sio kwenye chama.
Haya ni maamuzi ya kisisasa, sisi ndoa yetu ilifungwa kanisani haikufungwa kwa mwenyekiti wa chama au kwenye chama, kwa hiyo ndoa ni jambo jingine na harakati ni mjambo jingine, yeye ni mke wangu lakini haimaanishi tunakubaliana kwenye kila kitu, tunakubaliana kwenye mambo ya ndoa, kwenye siasa kila mtu anaweza akatazama jinsi anavyotazama yeye na sio shida”, amesema Kafulila.
Hivi sasa kumekuwa na mvutano kati ya wanandoa hao baada ya Kafulila kuhama CHADEMA, huku mke wake akisema hakuwa na taarifa zozote, na hata hizo sababu zake za kuhama hazina ukweli na kumtaka aweke wazi sababu rasmi za kufanya hivyo

No comments