Lema atapoteza muda wake - Gambo
Mrisho Gambo amefunguka na kusema Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema
anapaswa kutambua kuwa yeye kama Mkuu wa mkoa anajishughulisha na
matatizo ya watu hivyo kama hatabadili aina ya siasa azifanyazo basi
anapoteza muda wake kwa miaka mitano yote.
Gambo
amesema kuwa yeye hana tatizo lolote na Mbunge huyo wa Arusha mjini na
kudai kwamba anapaswa kutambua na kubadili aina ya siasa anazofanya kwa
kuwa yeye amelenga kutatua matatizo na changamoto za watu wa Arusha
Mjini.
"Msuguano na Mbunge haupo lakini anatakiwa tu asome alama za nyakati kwamba Mkuu wa Mkoa wa sasa amedhamiria kuhangaika na shida za watu kama hatalitambua hilo atapoteza muda wake kwa miaka yake yote mitano" alisema Mrisho Gambo
Aidha Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa yeye kama kiongozi kijana anahitaji zaidi kukosolewa kuliko kusifiwa ili aweze kujirekebisha sehemu ambayo ana mapungufu ili aweze kuwa kiongozi madhubuti na mahiri zaidi.

Post a Comment