TAMOBA: Wizi wa Pikipiki Dar Es Salaam sasa Basi
Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makore amewataka wa vyombo vya moto
kuzingatia sheria za usalama Barabarani wakati wawapo barabarani ili
kuepuka ajali zinazosababishwa na madereva wazembe na kuwataka kufanya
kazi kwa kuzingatia sheria zilizopo.
Mkuu
huyo wa Wilaya ameyasema hayo wakati wa uwekaji saini wa mkataba kati
ya Chama Cha Madereva na wamiliki Pikipiki Mkoa wa Dar es Salaam (CMPD)
na Kampuni ya Tanzania Motorcycle and Bajaji Association (TAMOBA)
kwaajili ya kuzisajili Pikipiki na Bajaji katika mfumo wa GPS
utakaowawezesha kujua Pikipiki iliyoibiwa ipo eneo gani na kuweza
kupatikana kwa haraka zaidi.
Nae
Afisa Utumishi wa TAMOBA Bw. Erasto Lahi amesema kwamba Kampuni ya
TAMOBA inatoza Shilingi mia moja kwa siku kwaajili ya kulinda Pikipiki
na Bajaji ya kila atakayesajiliwa na Kampuni hiyo kwa mfumo maalum wa
GPS utakaowezesha kujua Pikipiki iliyoibiwa ipo wapi, inatumiwa na nani
na kuwezesha kui-lock hapohapo ilipo.
“Mtu
aliye katika mfumo huu atapata msaada wa kulindwa kwenye mfumo muda
wote masaa 24, hivyo mmiliki wa chombo muda wowote akihitaji taarifa za
chombo kilipo, kilipopita na kinapoelekea atazipata, pia mfumo huu
utaunganishwa na Jeshi la Polisi moja kwa moja ili kuharakisha zaidi
huduma za kiusalama” Alieleza Bw. Lahi.
Hata
hivyo Bw. Lahi alieleza mfumo huo utasaidia kuokoa gharama za kulipia
Bima kubwa kwa kuwa kipengele cha hofu ya usalama wa chombo chake
kitafanyiwa kazi masaa 24 labda iwe kwa sababu zingine, mfumo huu
unawahakikishia wamiliki kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi watakuwa
salama.
Baada ya makubaliano ya pande zote mbili katika kusaini mikataba hiyo,Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makore alizindua kituo cha Chama cha
madereva na wamiliki wa pikipiki mkoa wa dar es salaam (CMPD),Na
kuahidi kuwapatia compyuta kwaajiri ya ofisi hiyo.
Post a Comment