Header Ads

Waziri awaonya Watumishi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amekemea vitendo vya wahamiaji haramu kuingia nchini kupitia mipaka ya nchi wakati mamlaka za kudhibiti vitendo hivyo zipo.
Ameyasema hayo kwenye ziara yake wilayani Misenyi mkoa wa Kagera katika mpaka wa Tanzania na Uganda (Mutukula) akikagua utendaji kazi wa idara ambazo zipo chini ya wizara yake na changamoto zinazowakabili kwa ajili ya kuzitatua ili kumaliza tatizo la wahamiaji haramu nchini.
“Wahamiaji kuingia nchini kwa kupitia kwenye mipaka yetu na kupenya hadi maeneo ya ndani ni udhalilishaji wa mamlaka zinazohusika”, amesema Waziri Mwigulu.
Aidha amewaonya watumishi wa Umma na wananchi wa wilaya ya Misenyi waishio karibu na mpaka wa Mutukula kutoshirikiana na wahamiaji kwani kufanya hivyo ni kosa kubwa na hatua kali zitachukuliwa juu yao.
“Lazima tupambane pia na watu wanaoshirikiana na waharifu na hii haibagui kama ni mtumishi ama si mtumishi ila ukiwa mtumishi adhabu yake inakuwa kubwa zaidi kwasababu unakuwa umekiuka sheria za utumishi”, ameongeza Waziri.

No comments