Mjadala wa Lissu ufungwe
Mkuu wa jeshi la polisi nchini, IGP Simon Sirro ametaka mjadala ufungwe
mara moja kuhusu sakata la mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu
kupigwa risasi na watu wasiojulikana mnamo Septemba 7, 2017 akiwa mjini
Dodoma.
IGP
Sirro ametoa kauli hiyo leo akiwa ziarani jijini Mbeya wakati
akizungumza na vikosi vya ulinzi na usalama ambapo amewaonya wanasiasa
kuacha kuuendeleza mjadala wa jambo hilo na waliachie jeshi la polisi
lifanye kazi yake.
Mbali na hilo IGP Sirro amewataka wananchi hususani wa mkoa wa Mbeya,
kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutii sheria
bila shuruti na kwamba, Jeshi la Polisi litahakikisha linawachukulia
hatua kali za kisheria ili kukomesha tabia hiyo.
Aidha Sirro amedai kuwa takwimu za uingizwaji na utumiaji wa dawa za
kulevya imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na kufanyika kwa operesheni
za mara kwa mara zinazofanywa na Jeshi hilo la polisi.
Post a Comment