Header Ads

Hamilton hakamatiki Formula1

Dereva wa timu ya Mercedes Lewis Hamilton ameendelea kupanua wigo wa alama kuelekea ubingwa wa dunia wa mbio za magari “Formula1”  dhidi ya mpinzani wake Sebastian Vettel wa Ferrari baada ya kushinda mbio za Japan (Japanese Grand Prix) mchana huu.
Muingereza huyo ameongoza mbio hizo zilizomalizika mchana huu nchini Japan akimuacha mbali mpinzani wake Mjerumani Sebastian Vettel ambaye alijiondoa kwenye mbio mapema baada ya gari yake kupata matatizo ya Injini.
Hamilton ameshika namba moja wakati namba mbili ikichukuliwa na Max Verstappen wa Red Bull huku Daniel Ricciardo wa Red Bull akishika nafasi ya tatu. Valtteri Bottas wa Mercedes ameshika namba nne wakati namba tano ikishikwa na Kimi Raikkonen wa Ferrari.

Hamilton sasa anaongoza kwa tofauti ya pointi 59 akiwa na pointi 306 dhidi ya Vettel mwenye pointi 247 zikiwa zimesalia mbio nne kumalizika kwa msimu huu.

No comments