Ujerumani yafuzu kwa Kombe la Dunia 2018
Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia
Ujerumani wamefuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Urusi
baada ya kulaza Ireland Kaskazini 3-1 mjini Belfast.
Sebastian
Rudy alifunga bao dakika ya pili, Sandro Wagner akaongeza la pili
baadaye, naye Joshua Kimmich akafunga la tatu mechi ikikaribia
kumalizika.
Josh Magennis alifungia Ireland Kaskazini bao la kufutia machozi kwa kutumia kichwa dakika za lala salama.
Ujerumani
wamefuzu wakiwa viongozi wa kundi lakini Ireland Kaskazini wanasalia
bado na matumaini ya kufuzu kupitia mechi za muondoano za kufuzu
Novemba.
Vijana hao wa Michael O'Neill watamaliza mechi zao Kundi C
nchini Norway Jumapili, wakilenga kumaliza wakiwa miongoni mwa timu
nane bora zitakazomaliza nafasi ya pili kati ya makundi tisa ya kufuzu.
Huenda wakahitaji alama moja Oslo kufika mechi za kufuzu za muondoano.
Droo ya mechi hizo itafanyika tarehe 17 Oktoba.
Post a Comment