Header Ads

Wazee kusakwa mitaani

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi amewaagiza watendaji wake kuwafuata Wazee waishio ndani ya wilaya hiyo kwaajili ya kuwasajili ili wapate huduma za matibabu bure.
Akiongea kwenye ziara yake ya kikazi DC Hapi amesema kuwa ameamua kutoka ofisini ili kuwafuata wananchi na kuongea nao juu ya changamoto na matatizo ili kuona namna ya kuyatatua.
Akiwa kwenye Kata ya Wazo Manispaa ya Kiondondi Hapi amefafanua kuwa yapo mambo mengi ambayo Serikali imeyatilia mkazo hasa suala la matibabu ya bure kwa wazee na utekelezaji wake unaendelea vizuri.
"Nimewaagiza watendaji wangu, wawafuate wazee kwenye Kata na Mitaa yao, ili wawatambue na kuwapatia kadi za msamaha wa matibabu, Serikali yetu imekwishasema wazee pamoja na watoto chini ya umri wa miaka mitano matibabu kwao ni bure, na hilo sina wasiwasi nalo kwa kuwa najua linatekelezeka", amesema Hapi.

Katika hatua nyingine Hapi amewataka wanachi kushirikisha serikali pale inapotokea kuwepo na michango isiyoeleweka, isiyofuata utaratibu wala kanuni za fedha ili matapeli hawa waweze kukomeshwa.

No comments