Header Ads

"Ni wale wale" - Lema

Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza baraza jipya la Mawaziri huku mawaziri wenfi wakiwa wamesalimika katika wizara zao na wachache kufanyiwa mabadiliko, Mbunge wa Arusha Mjini ametoa mtazamo wake na kusema kwamba katiba mpya
 ndiyo tumaini kwa nchi.
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Twitter, Lema amesema kwamba ameona mabadiliko ya baraza la Rais Magufuli lakini bado fikra ni zile zile na na watu ni wale wale na kudai katiba mpya ndilo suluhisho.
"Nimeona Mabadiliko Cabinet ya JPM. Watu ni wale wale, fikra zile zile. Katiba Mpya yenye fikra mpya ndio tumaini kwa mabadiliko sahihi ya nchi" Lema.

No comments