Header Ads

JUKATA kuandamana nchi nzima

Jukwaa la katiba nchini Tanzania (JUKATA) limetangaza kufanya maandamano ya amani nchi nzima, kutekeleza agizo la mkutano mkuu ili kurudisha hamasa ya mchakato wa katiba.
Taarifa hiyo imetolewa leo na wenyekiti wa JUKATA Bw. Hebron Mwakagenda alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, na kumtaka Rais ayapokee maandamano hayo na ujumbe wao, ukiwemo pia kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya.
"Kusudio la kufanya maandamano ya amani nchi nzima limetolewa na mkutano mkuu, mkutano ulituagiza kufanya maandamano  ili kuongeza hamasa, ili kuweza kurejesha mchakato wa katiba, tumemuomba Rais apokee haya maandamano kwa sababu ya mambo mawili, la kwanza ni kumpongeza kwa kazi nzuri anayoifanya, la pili ni kufikisha ujumbe wetu wa katiba, kwamba aturudishe kwenye mchakato", amesema Mwakagenda.
Mwakagenda ameendelea kwa kuomba na kulitaka Jeshi la Polisi kuwapa ulinzi wa kutosha siku hiyo, kwani wanalotarajia kulifanya ni suala la kisheria na lenye uzalendo, kwa ajili ya wananchi wa Tanzania, na kuwataka wananchi kushiriki kwenye maandamano hayo, ili kuunga mkono juhudi zao za kutaka kurudishwa kwa mchakato wa katiba na kupata muafaka wake.

No comments