Baraza jipya lawang'oa Kashililah, Maghembe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
amefanya mabadiliko kwenye baraza la Mawaziri ambalo ameongeza manaibu
mawaziri wapya watano na mawaziri wawili, panga lake
limewakata watano akiwepo Katibu wa Bunge Thomas Kashilillah
Ikiwa
ni kwa mara ya kwanza tangu alipoingia madarakani 2015 kufanya
mabadiliko ya baraza lake la mawaziri, panga la Rais Magufuli limempitia
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Thomas
Kashillilah ambaye nafasi yake imechukuliwa la Ndg. Steven Kagaigai
ambapo yeye ameambiwa atapangiwa kazi nyingine.
Aidha kutoa Kashillilah ambaye siyo
Waziri, Mawaziri walioachwa ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii,
Profesa Jumanne Maghembe na nafasi yake kuchukuliwa na Hamis Kigwangwala
aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Afya.
Katika panga pangua ya Rais, mwingine
aliyeachwa ni aliyekuwa Waziri Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson
Lwenge ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Katavi, Mhandisi
Issack Kamwele aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo.
Aidha aliyekuwa Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Ramo Makani naye panga hilo limepita na nafasi yake
kuchukuliwa na Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga.
Aidha aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura ambaye nafasi yake
imechukuliwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Juliana Shonza.
Rais Magufuli amewataka wale
walioteuliwa katika nafasi hizo kama watakuwa wamezipokea Jumatatu
atafanya shughuli ya kuwaapisha wateule hao.
Post a Comment