Mlemavu avamiwa akatwa mkono Morogoro
Katika kijiji cha Nyalutanga kata ya Kisaki mkoani Morogoro, Nasoro
Msingili ambae ni mlemavu wa Ngozi amevamiwa na watu wasiojulikana na
kumkata mkono wa kushoto na kutokomea nao ambapo tayari watu wawili
wanashikiliwa na Polisi mkoani humo.
Kwa
mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP. Leonce
Rwegasira amesema tukio hilo la kikatili limetokea Oktoba 3 majira ya
saa sita Usiku, katika Kijiji cha Nyalutanga, kilichopo Kata ya Kisaki
Wilayani Morogoro, na kwa sasa Bwana Nasoro Msingili amelazwa katika
kituo cha Afya Duthumi akiendelea kupatiwa matibabu huku tayari watu
wawili wakishirikiwa kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo.
Akizungumzia tukio hilo katibu wa chama cha watu wenye ulemavu wa
ngozi wilaya ya Morogoro Tatu Hussein ameitaka serikali kushirikiana na
wadau mbalimbali katika kuweka mikakati ya kudumu ya kukabilianana
matukio hayo
Kufuatia tukio hilo jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro limewataka
wananchi kuendeleza ushirikiano ili kuwabaini wote waliohusika katika
tukio hilo.
Post a Comment