"Marufuku kuwaweka ndani watumishi" - Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepiga marufuku tabia ya baadhi ya
viongozi katika maeneo mbalimbali nchini kuwakamata na kuwaweka ndani
watumishi wakiwemo wauguzi bila ya kufuata taratibu.
Waziri
Mkuu ametoa marufuku hiyo leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa
45 wa Chama cha Wauguzi Tanzania, mkoani Lindi ambapo amewataka wauguzi
nchini kufanya kazi kwa weledi, uaminifu pamoja na kufuata maadili ya
taaluma yao kwa kuwa maisha ya wagonjwa yako chini yao.
“Naagiza viongozi wote kufuata na kuzingatia sheria. Kama kuna makosa ya kitaaluma, Mabaraza husika yashughulikie jambo hilo na ni marufuku kuwaweka ndani watumishi kwa tuhuma za kitaaluma.”
Waziri Mkuu amesema kwamba katika sekta ya afya bila wauguzi ambao ni kundi kubwa kati ya Wanataaluma wa Afya, Serikali haitaweza kutekeleza ipasavyo mikakati mbalimbali iliyopangwa kwa ajili ya kuboresha sekta hiyo.
Katia hatua nyingine Waziri Mkuu amewaasa wauguzi wote nchini kuhakikisha wanazingatia kiapo cha maadili ya kazi yao na kwamba Serikali haitamvumilia yeyote atakae bainika kwenda kinyume.
“Nanyi Wauguzi mnao wajibu wa kutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia kiapo na miiko ya taaluma yenu. Tunazo taarifa kuhusu baadhi ya Wauguzi kutoa lugha chafu kwa wagonjwa, kuomba rushwa na wengine kujihusisha na vitendo vya wizi wa dawa.”
Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha afya za Watanzania wote zinaimarika ili kuendana na kasi ya utendaji kazi wa Serikali ya kuinua uchumi na kufikia wa kiwango cha kati, hivyo ni lazima watoe huduma bora kwa wananchi.
Pia amewaomba waunge mkono kwa nguvu zote jitihada za Serikali katika kuhakikisha miundombinu na vifaa vyote havihujumiwi na watu wachache ili viwe msaada mkubwa hususani kwa akina mama wajawazito ili wajifungue salama.

Post a Comment