Magufuli atilia mkazo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli
amezitaka Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) kuongeza wigo wa ukusanyaji
mapato ili waweze kuboresha huduma za jamii katika maeneo yao zikiwemo
za Afya na Elimu.
Rais
Dk. Magufuli amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam, katika Mkutano Mkuu
wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT), ambapo amesema bado maeneo
mengi kuna changamoto ya upungufu wa madarasa, pamoja na huduma za afya
ambazo zingeweza kutatuliwa kupitia mapato wanayokusanywa.
Aidha kiongozi huyo Mkuu wa nchi amesema
anakusanya changamoto ambazo mamlaka hiyo wanakutana nazo katika
ukusanyaji wa mapato kutokana na fedha nyingi kuishia mifukoni kwa
wachache, hivyo hawana budi kusimamia ukusanyaji huo wa mapato pamoja na
matumizi yake.
Mbali na hayo Rais Magufuli amewataka
Madiwani na Wakurugenzi kuwasisitiza kujiunga na katika mfuko wa Bima ya
Afya ili kuweza kupata huduma bora za kiafya ambapo pesa
zitakazookolewa zitaweza kufanikisha miradi mbalimbali.
Post a Comment