Rais awataka madiwani kujiuzulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,
amewataka madiwani wasio na shughuli ya kuwaingizia pesa binafsi
kujiuzulu, kwani serikali yake haiwezi kuwaongezea posho wanayohitaji.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa mkutano wa 33 wa Jumuiya Ya Tawala za Mitaa (ALAT)
uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es salaam, na kusema
kwamba Madiwani hao walifahamu masharti ya kugombea nafasi hiyo, hivyo
kama wameshindwa kuyatimiza ni vyema wakajiuzulu.
“Ndio maana diwani masharti tunapojaza fomu tunaambiwa lazima uwe na
kazi maalum inayokupa kipato, sasa kama wapo madiwani waliojaza hiyo
nafasi na hawana kazi ya kuwapa kipato, wajiuzulu udiwani”, amesema
Rais Magufuli.
Leo katika hotuba iliyowasilishwa kwa Rais Magufuli ikisomwa na
Mwenyekiti wa Jumuiya Ya Tawala za Mitaa (ALAT) Bwana Gulam Mkadam,
waliomba kuongezewa posho za madiwani, kutoka Tsh. 300,000 hadi Tsh.
800,000 jambo ambalo Rais amelipinga.
Post a Comment