"Wameshindwa kulipa kisasi" - Msuva
Winga wa Timu ya Taifa Stars, Simon Msuva amesema kwamba pamoja na
kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi katika mchezo wa
kirafiki leo anaamini kwamba timu hiyo ilikuja kulipiza kisasi cha
kipigo walichokipata katika michuano
COSAFA iliyofanyika nchini Afrika ya Kusini lakini wameshindwa.
Akizungumza baada ya mchezo uliochezwa
leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, Msuva amesema kwamba
wao walikuwa wamejiandaa kwa ushindi lakini haikuwa hivyo na hatimaye
kuangukia kupata sare ya bao moja ambalo alilifunga yeye mwenyewe katika
dakika 57 ya mchezo .
Katika mchezo huo ambao ulijaa
purukushani za kutosha ulimpelekea Kocha wa timu ya Malawi kutolewa
uwanjani kwa sababu ya kuvuka mipaka ya benchi la ufundi na kuingia
uwanjani wakati mechi ikiendelea.
Hata hivyo katika mchezo huo wachezaji
wawili wa Taifa Stars, Erasto Nyoni na Mzamiru Yassin walitolewa kwa
kadi nyekundu kutokana na makosa ya kimichezo yaliyoonekana na refa.
Kwa upande wa Malawi walitangulia kupata
goli katika dakika ya 35' kupitia Nahodha wa kikosi chao Ng'ambi Robert
ambapo alipofanyiwa mahojiano alisema "hajaridhishwa sana na goli
alilopata kwani alitegemea kufunga magoli zaidi ya mawili"
Post a Comment