Hasheem Thabeet kuweka historia
cheza
Kikapu Mtanzania Hasheem Thabeet, anatarajiwa kushuka dimbani kucheza
mchezo wake wa kwanza kwenye ligi ya Kikapu nchini Japan akiwa na timu
yake ya Yokohama B.
Hasheem
amesajiliwa na klabu ya Yokohama B, Septemba 28, mwaka huu
inayoshiriki Ligi Kuu ya mchezo wa kikapu nchini Japan ‘B1 League’
atatupa karata yake ya kwanza dhidi ya Levanga Hokkaido katika dimba la
kimataifa la Yokohama ‘Yokohama International Arena Pool’.
Mchezo huo wa kwanza kwa Thabeet ambaye
amewahi kucheza kwenye ligi ya Kikapu nchini Marekani (NBA) utapigwa
Oktoba 7 siku ya Jumamosi ya wiki hii.
Thabeet aliichezea klabu ya Oklahoma
City Thunder inayoshiriki ligi ya Marekani ‘NBA’ jumla ya michezo 224
ikiwa ni sawa na wastani wa pointi 2.1 na mitupo 2.6 “rebounds”.
Post a Comment