Tuna kazi ngumu - Kigwangalla
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Andrea Kigwangalla ambaye
jana ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii amefunguka na
kushukuru kwa kuaminiwa.
Kigwangalla
amesema jana alipata taarifa ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na
Utalii akiwa katika ziara ya Kituo cha Afya Kilimarondo Wilaya ya
Nachingwea hivyo ilibidi safari yake kuisha na kuanza kutoa namba za
gari lake kama Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
"Baada ya kupata taarifa
hiyo kila kitu ilibidi kisimame hapo hapo. Namba za NWAMJW ilibidi
ziondolewe na safari ya kutoka huko ianze! Nimepokea salamu nyingi za
pongezi na shukrani kwa Mungu aliye juu. Sintoweza kumjibu kila mtu,
uungwana ni kutambua pongezi zenu na dua tele mlizotuombea, nawashukuru
sana ndugu zangu. Tuzidi kuombeana dua tu" alisema Kigwangalla
Post a Comment