california ya waka moto
Maeneo ya jimbo la California, Marekani ambayo hukuza
mizabibu yameathiriwa na moto mkubwa ambao unaenea kwa kasi sana na
kusababisha vifo vya watu 10.
Mamia ya watu wamehamishwa makwao na inakadiriwa kwamba zaidi ya nyumba 1,500 zimeharibiwa na moto huo.
Watu saba waliuawa katika wilaya ya Sonoma, maafisa wamesema.
Watu zaidi ya 20,000 wamekimbia wilaya za Napa, Sonoma na Yuba baada ya moto mbaya zaidi wa nyika kuzuka maeneo hayo.
Gavana wa jimbo la California ametangaza hali ya dharura.

Post a Comment