Header Ads

Spika wa Bunge ajiuzulu kwa sababu

Spika wa Bunge la Ethiopia, Abadula Gemeda, amejiuzulu wadhifa wake huo bila kutoa sababu za maamuzi hayo.
Bw. Abadula ametangaza kujiuzulu kupitia televisheni ya taifa ya nchi hiyo, ameahidi kutoa sababu za maamuzi hayo katika tarehe ya baadaye.
Hata hivyo watu wengi wanadhani uamuzi wa Spika kujiuzulu ni hatua ya kupinga jinsi serikali kuu inavyoshughulikia hali ya usalama katika majimbo ya Oromia na Somali, ambapo watu wengi wameuwawa na maelfu kuondolewa kwenye makazi yao.

Spika wa Bunge ni miongoni mwa wanasiasa muhimu nchini Ethiopia na uamuzi wake wa kujiuzulu umewashangaza wengi. Kabla ya kuchaguliwa Spika, Bw. Abadula alikuwa ni Mkuu wa Jeshi, Waziri wa Ulinzi na pia Mkuu wa Jimbo la Oromia

No comments