Header Ads

Rais Magufuli abanwa kwenye adhabu ya kifo LHRC

Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu, LHRC kimemtaka Rais Magufuli kufuta sheria ya adhabu ya kifo kwani inachangia kupoteza rasilimali za nchi ikiwa ni pamoja na kutunza watu waliohukumiwa tangu mwaka 1994.
Akizungumza leo kwenye kuadhimisha kupinga adhabu ya kifo, Mkurugenzi mtetezi na maboresho ya Sheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za binadamu Bi. Anna Henga amesema kwa kuwa Rais aligoma kusaini wafungwa wanyongwe ndivyo anavyostahili pia kufuta vifungu vinavyoanisha sheria ya kunyongwa.
Bi. Mhenga amesema kwamba gharama zinazotumika kuwahifadhi watu waliopewa hukumu ya adhabu ya Kifo ni kubwa hivyo ni upotezaji wa rasilimali ambazo zingesaidia kufanyia shughuli mbalimbali.
Aidha ameongeza kwamba kwa utafiti uliofanyika haujawahi kupunguza matukio ya kihalifu kwani wafungwa hawapewi nafasi ya kwenda kurekebisha makosa yao kwa kuwa wanaishi kuhukumiwa kifo.
"Hii sheria ya hukumu ya kifo haimpi mtu nafasi ya kwenda kurekebisha makosa yake. Kwa ujumla haisaidii chochote kwani ukigalia kuna watu kibao walihukumiwa kifo hawajapata nafasi ya kurekebisha makosa yao ya awali. Lakini pia hata pamoja na kwamba adhabu hii inatolewa bado matukio bado yanaongezeka kila siku....Bi Henga ameeleza
Adhabu za vifo nchini hazitekelezwi lakini yamerudi kwa sura tofauti kama mauaji ya watu wenye ulemavu. Mfano mtua anayetenda mauaji ameyaona maisha hayana thamani hivyo kama serikali na yenyewe itatekeleza adhabu ya kifo na yenyewe itakuwa imeungana kuona kwamba maisha hayana thamani kama muuaji.
Leo Kituo cha Sheria na Haki za binadamu LHRC imeungana na Mtandao wa kupinga adhabu za kifo Duniani kuadhimisha miaka 15 ya Siku ya kupinga adhabu hiyo.

No comments