Serikali yatoa Miezi 3 kwa wananchi
Wanakijiji 1,830 wa kijiji cha Bwila Chini Mkoani Morogoro wapewa miezi
mitatu kuhama Wananchi zaidi ya 1,800 wa kijiji cha Bwila Chini na
Kiburumo tarafa ya Mvuha Wilaya ya Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Stephen
Wakazi
hao wametakiwa kuondoka katika eneo hilo ndani ya kipindi hicho kwa
ajili ya kupisha ujenzi wa bwawa katika eneo hilo baada ya kulipwa fedha
zao za fidia na kumalizika kwa msimu wa Mavuno.
Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa malipo ya fidia awamu
ya pili katika viwanja vya Shule ya Msingi Bwila Chini, Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro, Dk. Kebwe Stephen Kebwe, amesema lengo la Serikali ni kutaka
wananchi hao kupata makazi mapya baada ya kutakiwa kupisha ujenzi wa
bwawa katika eneo hilo hivyo ni vyema wakatumia kiasi hicho cha fedha
kama ilivyoelekezwa.
Kwa upande wake, Meneja Miundombinu Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
Mkoa wa Morogoro ,Mhandisi John Kirecha, amesema, malipo hayo
yanatokana na malalamiko yaliyoibuka wakati wa malipo ya awamu ya kwanza
mwaka 2014 ambapo jumla ya shilingi Bilion 4 zinatarajiwa kulipwa kwa
wananchi zaidi ya 1,800.
Post a Comment