MAFISADI WACHOMWA NA KUBENEA
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage amesema
wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki waliobinafsisha kiwanda
hicho na kuiingizia hasara serikali watashughulikiwa ipasavyo.
Mwijage
ameyasema hayo bungeni leo wakati akijibu maswali mawili ya nyongeza
yaliyoulizwa na mbunge wa Ubungo Mh. Said Kubenea aliyetaka kujua hatua
watakazo chukuliwa wafanyakazi walioshiriki kubinafsisha kiwanda cha
urafiki kwa mwekezi kutoka China ambaye ameshindwa kuleta faida.
“Ukiiona ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG utalia Kubenea, kwahiyo kila mtu aliyehusika kutuingiza kwenye dhahama hii rungu litamshukia kama Mwewe”, amesema Waziri Mwijage
.
Aidha Waziri amesema kuwa tayari serikali ipo mbioni kumaliza makubaliano na mwekezaji mpya kutoka China ambapo kiwanda hicho kitajengwa upya vizuri na serikali itanufaika kwa takribani asilimia 75.
Waziri Mwijage ameongeza kuwa kiwanda cha Urefiki ni cha kihistoria hivyo watakijenga upya na kitakuwa na wafanyakazi zaidi ya elfu nane.

Post a Comment