NAPE MIMI SIPO KAMA NYALANDU
Mbunge wa Jimbo la Mtama (CCM) Nape Nnauye amefunguka kutokana na
tetesi zilizokuwa zikizagaa na kuzungumzwa kuwa naye yuko mbioni kuhama
chama chake cha mapinduzi kama ambavyo amefanya Lazaro Nyalandu.
Nape kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost picha ambayo wako watatu akiwemo yeye, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, na aliyekuwa Mbunge wa Singida kupitia CCM ambaye amejivua uanachama , Lazaro Nyalandu.
Baada
ya kuweka picha hiyo Mh. Nnauye ameandika maneno ambayo yanaonesha hana
mpango kabisa wa kuhama chama chake kama ambavyo inahisiwa na watu
mbali mbali.
“Chama
cha siasa ni itikadi, itikadi ni imani. Siamini sana katika kubadili
imani kienyeji. Nitashughulikia mapungufu nikiwa ndani na sio nje!”
Ameandika Nape
Kufuatia
Mh Nape Nnauye kuonesha msimamo wake huo, hatua hii moja kwa moja
itafunga majadiliano ya watu katika sehemu tofauti kuwa ana mpango wa
kukitosa chama cha CCM.
Post a Comment