MAJIBU YA MAJALIWA KUHUSU KATIBA MPYA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema
kuwa Changamoto za jamii ni nyingi kuliko mahitaji ya Katiba hivyo suala
la katiba sio kipaumbele cha serikali kwa sasa
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo Bungeni wakati wa kipindi cha maswali kwa
Waziri Mkuu, ambapo alijibu swali la Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea
lililohoji kuwa ‘Serikali ya awamu ya tano imetimiza miaka miwili lakini
hakuna jitihada zozote zilizofanywa katika kuendeleza mchakato wa
katiba ulioachwa na Serikali ya awamu ya nne.
Akijibu
swali hilo Waziri Mkuu amefafanua, “Katiba mpya inahitaji gharama kubwa
na sisi tumeanza na kutatua changamoto za jamii kwanza, ikiwemo
mahitaji ya maji, changamoto za elimu, na sekta ya Afya”. Amesema Waziri
Mkuu
Waziri
Majaliwa ameongeza kuwa Katiba ni muongozo tu na wakati ukifika
serikali yake imemaliza changamoto basi wataanza mchakato huo.
“Kila
bajeti ina vipaumbele vyake, kwa sasa acha tufanyie kazi vile ambavyo
vinasumbua wananchi wengi kwani kipaumbele kikuu ni kuimarisha huduma za
jamii hivyo tunasimamia ukusanyaji mapato ili tumalize changamoto hizi
na katiba ni muongozo tuu acha tutumie huu uliopo sasa”. Amesema Waziri
Mkuu
Post a Comment