Pingamizi la Lipumba latupwa Mahakamani
Chama Cha Wananchi (CUF) kimeshinda pingamizi dhidi ya Mwenyekiti wa
CUF Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na Msajili wa Vyama Vya Siasa
nchini na watu wake katika kesi ya bodi ya Udhamini - RITA
Leo
Oktoba 5, 2017 katika Mahakama Kuu mbele ya Jaji Wilfred Dyansobera
imetoa maamuzi juu ya mapingamizi yaliyowekwa na Lipumba aliyekuwa
akiwakilisha na Wakili Mashaka Ngole na Majura Magafu akiwemo
Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Shauri (Namba Miscilleneous Civil
Application No. 51/2017) kuhusu CUF kuomba kuwazuia Wajumbe wa Bodi ya
Wadhamini iliyosajiliwa na Lipumba wasifanye kazi ya Bodi hiyo mpaka
pale shauri la msingi Namba 13/2017 litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi
na Mahakama Kuu.
Jaji Wilfred ameyatupilia mbali mapingamizi hayo kutokana na kutokuwa
na hoja za msingi za kisheria. Mhe Jaji amekubaliana na hoja
zilizowasilishwa na Mawakili upande wa CUF unaomuunga mkono Katibu Mkuu
wa chama hicho akiwepo Mhe Fatma Karume, na Mhe. Mpoki Kabe.
Kufuatia maamuzi hayo yanatoa nafasi ya kwenda kusikilizwa kwa undani
wa hoja zilizowasilishwa Mahakamani hapo na Ally Salehe ambaye ndiye
muombaji
Hoja za pande zote mbili zitawasilishwa kwa maandishi kwa utaratibu
mpaka Oktoba 19, 2017 Ally Salehe ambaye ni muombaji anapaswa kuwa
amewasilisha huku Oktoba 17, 2017 upande wa walalamikiwa wanapaswa kuwa
wawe wamejibu na mnamo Novemba 6, 2017 Ally Salehe awasilishe majibu
zaidi na tarehe 7, Novemba kesi itatajwa kwa kupagwa siku ya kutolewa
Maamuzi.
Post a Comment