Header Ads

Mke wa Rais aonya Rais kupinduliwa

Mke wa rais wa Zimbabwe Grace Mugabe ameonya juu ya uwezekano wa mipango ya mapinduzi kufuatia kuongezeka kwa  mtafaruku wa mapambano ya mtu atakayemrithi mume wake rais wa nchi hiyo Robert Mugabe.
Grace Mugabe amesema wafuasi wa Makamu wa rais Emmerson Mnangagwa wanawatishia maisha wale ambao hawamuungi mkono makamu wa rais ili kumridhi rais Mugabe ambaye ana umuri wa miaka 93.
Taarifa zinasema Bi Grace Mugabe na Makamu wa rais Mnangagwa ndiyo wanaotajwa kuwa wapinzani kuwania nafasi hiyo na kuweka makundi ndani ya Chama tawala cha Zanu-PF.
Wafuasi wa Makamu wa rais wamedai kwamba wapinzani ndani ya chama tawala cha Zanu-PF walihusika ingawa makamu wa rais amejitenga na tuhuma hizo na kuliambia shirika la habari la taifa nchini humo kuwa bado ni mwaminifu kwa rais.

No comments