Header Ads

Kocha wa kwanza kutimuliwa VPL

Kocha Mkuu wa kikosi cha Njombe Mji kilichopanda ligi kuu Tanzania Bara msimu huu Ahmed Banyai amefutwa kazi leo baada ya matokeo mabaya iliyopata timu hiyo katika mechi zake tatu za mwanzo.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa Banyai hataendelea na majukumu yake kutokana na timu hiyo kushindwa kupata matokeo mazuri katika mechi zake tatu ambapo imepoteza zote.
Kocha msaidizi wa timu hiyo Mrage Kabange huenda akachukua mikoba ya Banyai. Njombe Mji inashika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi ikiwa haina alama hata moja sawa na Stand United ambazo zote zimefungwa mabao 3 katika michezo yao mitatu. 

No comments