Header Ads

MUGABE AJITOKEZA HADHARANI

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amejitokeza kwa mara ya kwanza hadharani tangu Jeshi la nchi yake litangaze kuchukua madaraka huku likikanusha kufanya mapinduzi.
Rais Mugabe ameonekana kwenye mahafali ya chuo kimoja jijini Harare baada ya kuwa chini ya kuzuizi cha nyumbani kwa siku kadhaa huku kukiwa na mvutano kuhusu ni nani atamrithi.
Jeshi limesema limekuwa kwenye mazungumzo na Mugabe na litaujulisha umma kuhusu matokeo ya mazungumzo wakati wowote.
Jeshi lilichukua udhibiti wa nchi baada ya Rais Mugabe kumfukuza kazi Makamu wa Rais, Emmerson Mnangagwa, wiki iliyopita, hatua iliyoashiria uwezekano mkubwa wa mkewe Bi Garce kuchukua uongozi wa Chama tawala, Zanu-PF na urais.

No comments