Header Ads

Lema ashauri Waziri akapimwe mkojo

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameshauri Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba akapimwe mkojo kutokana na kuwa na wasi wasi na kauli zake ambazo amekuwa akitoa katika mikutano ya hadhara.
Lema amesema kwamba anafahamu kwamba kiongozi huyo hatumii dawa za kulevya au kilevi chochote lakini amekuwa akimtilia mashaka kutokana na kauli zake.
"Nafahamu Mh Mwigulu atumii madawa ya kulevya au kilevi chochote,lakini kauli zake kwenye mikutano ya hadhara ya kampeni za udiwani zinaleta wasi wasi nakuona ni vyema nikashauri apimwe mkojo" Lema.
Aidha Lema ameongeza kwa kuhoji  "Anasema eti kupigwa Lissu risasi hakuna mahusiano na kuomba kura"?

No comments