Dully ataja urithi alioachiwa na baba yake
Msanii Dully Sykes ambaye hapo jana ameachia wimbo wake mpya wa
'Bombadier', amesema marehemu baba yake amemuachia urithi mkubwa ambao
ni muhimu sana maishani mwake.
Akiongea
kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dully Sykes amesema
anajivunia kitendo cha baba yake kumuachia urithi wa 'nguvu', kwani
ameweza kuwa na watoto wengi.
"Kitu ambacho mzee ameniachia na najivunia ni kuwa na nguvu za kuwa
na watoto wenGi, tayari nina watoto wengi na bado wengine watakuja”,
amesema Dully Sykes.
Baba Mzazi wa Dully Sykes ,ambaye pia alikuwa msanii na kipenzi cha
watu, Mzee Abby Sykes alifariki dunia Februari 15, 2015, baada ya kuugua
muda mrefu.
Post a Comment