CUF yaikana UKAWA
Chama cha CUF upande wa Prof. Ibrahim Lipumba, kimesema hawautambui
umoja wa vyama vya upinzani nchini (UKAWA) na hawana mpango wa
kushirikiana nao kwenye uchaguzi ujao.
Taarifa
hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Abdul
Kambaya, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, na kusema kwamba
chama hicho hakioni sababu yoyote ya kushirikiana na vyama vingine
kwenye uchaguzi huo unaohusisha halmashauri 34.
“CUF tunashiriki kwenye uchaguzi huu lakini hatututegemei kushirikiana na umoja wowote ule, sisi hatuitambui Ukawa lakini tunajua kuna vyama vingine, tuko tayari kuelekea kwenye uchaguzi huo bila kuhusishwa na chama kingine chochote, na tunaamini tutafanya vizuri”, amesema Kambaya.
Hii ni mara ya kwanza kwa chama hicho kuweka msimamo wake kuhusu uchaguzi tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka 2015, na mgogoro uliopo baina yao na wanachama wengine wa CUF wanao muunga mkono Sheikh Sharif Hamad.

Post a Comment