Header Ads

Bidhaa za nje mwisho Disemba

Jumuiya ya Afrika Mashariki imepanga kudhibiti ubora wa bidhaa za Afya zinazoingizwa katika nchi zake kutoka mataifa mbalimbali ili kuendana na ubora ambao unatambuliwa na nchi hizo.


Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya kwenye mkutano unaojadili uainishaji wa kanuni za ushughulikiaji wa dawa pamoja  na vifaa tiba kwa nchi za Afrika mashariki.
Dkt. Ulisubisya amesema Jumuiya inataka kuweka utaratibu kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa na utaratibu wa kuleta bidhaa za afya kutoka nchi zenye viwango vya ubora unaofanana na wa nyumbani.
“Lengo la Jumuiya ni kwamba ifikapo mwishoni  mwa  mwaka huu (2017) bidhaa yoyote inayoingia  katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki  ziwe na ubora unaofanana kulingana na ubora wa nchi zilizopo ndani ya Jumuiya”, amesema Ulisubisya.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA) Hiiti Sillo amesema mifumo ya udhibiti nchini Tanzania ni mifumo inayoongoza  huku akisema kuwa makubaliano  yaliyopo ni kwamba mifumo yote ni lazima iwezekukidhi  viwango vya ubora huku nchi za Kenya  na Uganda zimesema  kufikia  mwezi  Disemba mwaka huu zitakuwa  zimefikia kwenye viwango vya ubora huo.

No comments